Verse 1
hii ni kama kumbu kumbu ya torati
washasoma zaburi mara mbili ndo tamati
wamekata tamaa ya kumwona mama tena
wanakumbuka sauti ya baba mwaka jana
aliposema eee wanangu mimi sitapona tena
wanalia machozi waliyobakiza jana
wakikumbuka ndugu mali walivyogawana
kwa hasira wanahisi hawana thamani tena
wanasema bora kufa kuliko kuishi sana
wangependa kusoma ila ada hazijatimia
wameshafukuzwa shule wako chimbo wanalia
hawana rafiki, mungu ndo rafiki
ndugu wanafiki mambo yakisanda
wanaweza saidia jeneza na sanda
washasahau kulala juu ya vitanda
sauti za mbu wa usiku kwao ndo vinanda
Chorus
tuna ndoto za kuwa ma doctor
tuna ndoto za kuwa ma pilot
tuna ndoto nyingi za maisha
tuwezeshwe tunaweza
tuna ndoto za kuwa ma doctor
tuna ndoto za kuwa ma pilot
tuna ndoto nyingi za maisha
tuwezeshwe tunaweza
0 Comments