''Nimekuchagua Wewe'' by Bob Rudala


Nimekuchagua wewe, uwe wangu

Verse 1
Ni safari ndefu, ya mwanadamu
Maisha na mapenzi, uwe mke ama mume
Mara moja kubahatika, maishani mwako
Kumpata mtu fulani, ambaye huwa ni maalum kwako
Kipenzi cha moyo wako, kati ya dhiki kubwa
Nimetambua na kuamini, kuwa kukutana kwetu
Mwanzo wa kutimia, kuwa ile ndoto yangu
Ya siku nyingi, kwani pendo letu linakua
Kulingana na wakati, kila siku maishani mwangu
Nilikuwa na ndoto, ya kumpata wangu mwenzi
Tufunge naye pingu za maisha

Chorus
Nimekuchagua wewe, uwe wangu
Wangu wa maisha, wa kufa na kuzikana
Sijali mengi maneno watu wasemayo
Yaliyopita si ndwele, tugange yanayokuja
Nimekuchagua wewe, uwe wangu
Wangu wa maisha, wa kufa na kuzikana
Sijali mengi maneno watu wasemayo
Yaliyopita si ndwele, tugange yanayokuja

Nakupenda wewe, malaika wa moyo wangu
Nakuhusudu wewe, ua la moyo wangu (Mama mia)
Moyoni nina furaha tele, upo mikononi mwangu

Verse 2
Na kwa pete hii, ninakuoa
Uwe mke wangu wa ndoa
Hakika wewe ni ubavu wangu
Kwa penzi nimefika, kama meli
Nimetia nanga kwako, pengine kato sitamani
Umewaacha wazazi wako, baba na mama
Kwa mapendo umeungana nami
Katika ndoa takatifu, na leo si wawili tena
Tu mwili mmoja, tumwwombe Mungu atujalie
Ndoa yenye baraka, tuje tuzae na watoto
Waizunguke meza yetu, upendo utawale nyumba yetu
Tuwe wa wakarimu kwa wageni wetu wote

Chorus
Nimekuchagua wewe, uwe wangu
Wangu wa maisha, wa kufa na kuzikana
Sijali mengi maneno watu wasemayo
Yaliyopita si ndwele, tugange yanayokuja
Nimekuchagua wewe, uwe wangu
Wangu wa maisha, wa kufa na kuzikana
Sijali mengi maneno watu wasemayo
Yaliyopita si ndwele, tugange yanayokuja


Post a Comment

0 Comments