Verse 1
Eti nikuombee mema
Na baraka uzidi fanikiwa
Siwezi kamwe wala
Ni sawa na kuiforce sinema
Kuitazama na haijanivutia
Lazima tu ntalala
Na kwa barabara ukipita
Nenda kulia ukiniona kushoto
Sitaki hata tuonane
Usije wala ukaniita
Donda vilia utanchochea tu moto
Nisije nkutukane
Bridge
Kinachoniumiza nafsi
Kunisikitisha kwa watu kujishongondoa
Kumbe mapenzi Hisabati wakati nayazidisha
Mwenzangu Nje unayatoa
Wewe cement mimi mchanga
Nkasema Penzi tujenge lisije loa
Najitia mkandarasi naezeka mabati
Wewe chini kenchi unabomoa
Chorus
Niache
Niache
Niache Oh Niache
Niache
Nipambane na moyo wangu
Niache (Niaaa)
Niache (Moyo wangu una hasira)
Niaache Oh Niache
Niache
Verse 2
Najitahidi nisilale kwenye kitanda
Huenda ntapunguza ndoto zako
Mwilini nina machale utadhani mwanga
Yote kuusahau uwepo wako
Laiti kama ningekuwa gari
Ningekugonga barabarani
Ama nyuki mtoa asali
Nkung'ate sura wasiitamani
Hivi wewe ungo ulivunja mwali
Ama ulivunja sahani
Kuniundia mateam kwa mitandao
Vijembe vya kazi gani
Bridge
Kinachoniumiza nafsi
Kunisikitisha kwa watu kujishongondoa
Kumbe mapenzi Hisabati wakati nayazidisha
Mwenzangu nje unayatoa
Wewe cement mimi mchanga
Nkasema penzi tujenge lisije loa
Najitia mkandarasi naezeka mabati
Wewe chini kenchi unabomoa
Chorus
Niache Oooh Niachee
Niache (Mimi moyo wangu una hasira)
Niache (Tena ukae mbali)
Niache (Oooh niachee)
Niache (Usiwapigie rafiki zangu)
Niache (Usithubutu hata simu yangu)
Niache (Chonde tafadhali)
Niache (Niaaa)
Outro
Iyoo Lizer
Hhhhmm
Ntakudanganya kwa tabasamu
Ntakudangany kwa kucheka
Ntakudanganya hata kwa salamu
Ila moyoni nakuchukia
Nitakudanganya kukufollow
Nitakudanganya kucomment
Nitakudangaya kulike picha
Ila siwezi kukuzimia
Mxiuuuuu
0 Comments