"Acha Nikae Kimya" by Diamond Platnumz


Mama ananiambia Nasibu mi ni
Mtu mzma nawe ndo nakutegemea
Yanayotokea jaribu kupiga kimya
Usidiriki ata kuongea
Mara nasikia vya aibu Konda Gwajima
Eti ugomvi umekolea
Kuchunguza karibu ni binti mmoja
Kwa mitandao anachochea
Najariibu kunyamaza ila moyo hautakii
Unanambia eti Simba japo unguruma uisemee hakii
Ooh najaribu kunyamaza ata Lizer ataki yooh
Anasema walau nena kidogo hiih

Na mashabiki Dangote
Wananambia mbona husemi chochote ah
Si uko nao siku zote
Ama ulezi unafanya uogope ah
Na media pande zote
Wanalalama kiongozi atoke eh
Nchi inaingia matope
Niende wapi na mi mtoto wa wote
Yaani lawama

Wacha nikae kimya
Mmh nisiongee (Kimya)
Ooh ninyamaze mimi (Nikae kimya)
Nisiseme (Kimya)
Mama kaniambia (Wacha nikae kimya)
Ooh nifunge mdomo (Kimya)
Mie bado mdogo sana (Nikae kimya)
Nisiseme (Kimya)

Mmh ni mengi majaribu
Najitahidi epuka yasije nicost
Japo mengine swadakta mengine hayana maana
Rafiki kipenzi wa karibu
Hata nyimbo yake sikuweza ipost
Ila alivokamatwa iliniumiza sana
Mitandaoni kila kona
Uongo na ukweli unashonwa
Kila nyumba inanong'ona
Ah oh Tanzania
Mara kimbembe Dodoma
Bunge upinzani wamegoma
Juzi akapotea na Roma
Ohh Tanzania

Najaribu kunyamaza
Makame hataki yooh
Ananiambia walau nena kidogo
Nyumbani nafungua gate
Niende kwa Mangi nunua supergate eh
Napewa za chini ya carpet
Kuna radio imevamiwa eti eh
Napita kwenye (Magazeti)
Nakuta rundo la watu (Wameketi) eh
Badala ya kutafuta cent
Wanabishana tu mambo ya vyeti

Wacha nikae kimya
Ooh nisiongee (Kimya)
Ninyamaze Kabisa (Nikae kimya)
Eh! ulimi koma! (Kimya)
Usije kunipoonza!(Acha nikae kimya)
Nifunge bakuli langu! (Kimya)
Nikojoe nikalale! (Nikae kimya)
Mi bado mdogo sana (Kimya)
Mama kaniambia

Oh najiuliza (Waaaapi)
Najiuliza (Waaaapi)
Tunakwenda wapi (Waaaapi)
Kila siku maneno (Waaaa)
Ah tuacheni jamani (Waaapi)
Mi na we ni taifa moja (Waaapi)
Kambarage baba mmoja (Waaaapi)
Sa tofauti za nini (Waaa) tushikamane tukaijenge Tanzania

Post a Comment

0 Comments